KITABU; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.

July 7, 2016

Karibu rafiki upate kitabu MIMI NI MSHINDI, Ahadi yangu na nafsi yangu. Kitabu mimi ni mshindi kinakuwezesha wewe kuishi maisha ya ushindi, maisha ambayo yanakutofautisha wewe na wengine wengi ambao wanashindwa kufikia mafanikio makubwa.

Ukiangalia maisha ya washindi na maisha ya wale ambao wanashindwa yapo tofauti kabisa. Kuna namna ambavyo washindi wanachukulia mambo yao, wanavyotumia muda wao, wanavyotengeneza mahusiano yao na pia wanavyoshirikiana na wengine. Washindi wana njia tofauti za kuweka malengo ambayo wanayafikia na hivyo kuendelea kuwa washindi.

read more

KITABU; BIASHARA NDANI YA AJIRA, JINSI YA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA YAKO UKIWA BADO UMEAJIRIWA.

June 11, 2016

KITABU BIASHARA

BIASHARA NDANI YA AJIRA ni kitabu ambacho kinakupa mbinu za kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa. Ni kitabu ambacho kila mwajiriwa anapaswa kukisoma kwa sababu kina maarifa muhimu ya kumwezesha mwajiriwa kujikomboa kiuchumi.

Wote ni mashahidi kwamba hali ya ajira kwa sasa imebadilika sana. Na kipato cha ajira kimekuwa hakitoshelezi. Na hata zile njia ambazo watu walikuwa wanatumia kujipatia kipato cha ziada kama posho, marupurupu na hata rushwa kwa sasa vimedhibitiwa kwa kiasi kikubwa.

read more

KITABU; KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, TOLEO LA KWANZA 2016.

June 11, 2016

KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, TOLEO LA KWANZA 2016.

Habari njema kwa wana mafanikio wote, kitabu chako ambacho ndio mwongozo wa maisha ya mafanikio kwa mwaka huu 2016 tayari kimetoka. Kitabu hiki kinaitwa KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO.

Hiki ni kitabu ambacho kinakupatia wewe maarifa sahihi ya kuishi maisha ya mafanikio, kwa vyovyote vile unavyoyapima mafanikio kwenye maisha yako. Safari ya mafanikio sio rahisi, kuna changamoto na vikwazo vingi, kuna kushindwa na kukatishwa tamaa na pia kuna kujisahau pale ambapo unakuwa umeshayapata mafanikio.

read more

KITABU; JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

June 11, 2016

JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

Kama kuna kitu kimoja ambacho tuna uhakika nacho hapa duniani ni kwamba dunia inabadilika kila siku. Ukiangalia historia ya dunia tulikotoka na tulipo sasa kumetokea mabadiliko makubwa sana. Zilianza zama za mawe, zikaja zama za chuma, yakaja mapinduzi ya viwanda na hata sasa tupo kwenye mapinduzi ya kiteknolojia.

Jambo moja la kushangaza ni kwamba pamoja na mabadiliko haya kuwa wazi bado watu wengi ni wagumu sana kubadilika. Watu hawapendi mabadiliko, wanapenda kufanya kile walichozoea kufanya na wanataka maisha yaendelee vile yalivyokuwa jana na leo. Kitu ambacho ni ndoto isiyowezekana.
Katika zama zote ambazo dunia imepita, kuna watu ambao waliweza kubadilika haraka na kupata faida ya mabadiliko, wengine walilazimishwa kubadilika na hivyo kuburuzwa na kuna ambao waliachwa na mabadiliko na hivyo kupotea. Waliofaidika na mabadiliko ni wale waliokuwa tayari kubadilika, walioburuzwa na mabadiliko ni wale ambao walikuwa hawajui kama kuna mabadiliko ila wanakwenda tu na hali ilivyo. Walioachwa na mabadiliko ni wale ambao hata baada ya kuona mabadiliko wao waligoma kubadilika, waliendelea kung’ang’ania kile walichozoea na hatimaye kuachwa nyuma na kupotea.

read more

KITABU; JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG.

June 11, 2016

JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG.

Tunaishi kwenye ulimwengu wa zama za taarifa. Katika ulimwengu huu wale wenye taarifa sahihi ndio wanaonufaika kuliko wale ambao hawana taarifa sahihi. Pia katika ulimwengu huu taarifa watu wengi wameweza kunufaika kwa kuuza taarifa ambazo wanazo na wengine wanazihitaji.

Je na wewe upo tayari kunufaika na taarifa ulizonazo, ambazo zinaweza kuwanufaisha wengine? Kama jibu ni ndiyo basi kuna njia moja nzuri kwako kuweza kuuza taarifa zako kwa wengine. Na njia hii ni kumiliki blog ambayo unaweza kuiendesha kibiashara.

read more

KITABU; KWA NINI MPAKA SASA WEWE NI SIO TAJIRI.

June 11, 2016

KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI

Madhumuni ya kuandika kitabu hiki ni kuwasaidia wale wote wenye

malengo ya kufanikiwa kwenye maisha yao na kuwa matajiri. Kwa

bahati mbaya sana kwenye mfumo wa elimu hakuna sehemu ambapo tunafundishwa somo linalohusiana na kutengeneza utajiri.

Wachache wanaojua siri za kupata utajiri wamekuwa wakinufaika nazo na wengi ambao hawajui siri hizi wamekuwa wakiteseka kila siku kuendesha maisha yao.

Kupitia kitabu hiki utajifunza sababu ishirini na tano ambazo zinakuzuia wewe kuwa tajiri. Na kwa kila sababu utakayojifunza utapewa hatua za kuchukua ili kuweza kuondokana na sababu hiyo na kufikia utajiri.

read more